Maguire Kuwakosa Bayern Kesho

Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Harry Maguire atakosekana katika kikosi cha Manchester United kitakachosafiri kuelekea Ujerumani kuwakabili Bayern kutokana na majeruhi.

Maguire alionekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake leo katika uwanja wa mazoezi wa Carrington lakini taarifa rasmi kutoka klabuni zimeeleza kua beki huyo hatakuepo kwenye kikosi kitakachoenda Munich kutokana na majeraha.maguireBeki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye siku za hivi karibuni amekua akipokea ukosoaji mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo,Lakini ameendelea kua imara na kuhakikisha anarudisha ubora wake.

Taarifa nzuri kwa mashabiki wa Manchester United baada ya beki Maguire kukosekana katika mchezo wa kesho dhidi ya Bayern ni urejeo wa beki wa kimataifa wa Ufaransa Raphael Varane ambaye alikosekana katika michezo kadhaa iliyopita.maguireManchester United ambayo inatarajia kusafiri leo kuelekea jijini Munich kumenyana na klabu ya Fc Bayern kesho inatarajia kwenda na mabeki wanne wa katikati ukiachana na raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye amepata majeraha na mabeki hao ni Lisandro Martinez, Victor Lindelof, Raphael Varane, pamoja na Johny Evans.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.