Amrabat, Mainoo Warejea Mazoezini

Viungo wa klabu ya Manchester United Sofyan Amrabat na kinda Kobbie Mainoo wameelezwa kurejea mazoezini katika klabu hiyo baada ya kua nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Amrabat na Mainoo wameonekana katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya Manchester United unaofahamika kama Carrington, Hii ikiwa ni taarifa nzuri kwa benchi la ufundi la klabu hiyo pamoja na mashabiki wa klabu hiyo.AmrabatKiungo Amrabat yeye amejiunga na Manchester United akitokea Fiorentina ilielezwa alikua na majeraha madogo ambayo yalimfanya kukosa mchezo wa wikiendi iliyomalizika ambao alionekana akiwa jukwaani.

Taarifa ya klabu hiyo ilieleza wazi viungo hao wamefanya mazoezi ya peke yao na hawajajumuika na wenzao ili kuangalia utimamu wao kabla hawajajumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo moja kwa moja.AmrabatKiungo kinda Kobbie Mainoo alianza vizuri sana katika michezo kadhaa ya kujiandaa na msimu na kuonesha kiwango kizuri kabla ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Real Madrid mnamo mwezi wa Saba ambapo amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili.

Acha ujumbe