Reece James Ashtakiwa na FA

Shirikisho la soka nchini Uingereza limemshtaki beki wa kulia wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James kwa kutoa lugha zisizo za kiungwana dhidi ya mwamuzi.

Beki Reece James inaelezwa alitoa lugha zisizo za kiungwana dhidi ya mwamuzi katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu yake dhidi ya klabu ya Aston Villa siku ya jumapili Septemba 24 mchezo ambao walipoteza kwa goli moja kwa bila.Reece jamesBaada ya mchezo inaelezwa beki huyo alimtolea mwamuzi wa mchezo huo Jarred Gillet maneno makali wakati wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge.

Beki huyo amevunja kanuni ya shirikisho inayofahamika kanuni namba E3 ambayo mchezaji haruhusiwi kutoa maneno yeyote yasiyo ya kiungwana na beki huyo alijikuta akiingia kwenye mzozo na mwamuzi huyo na kumfanya kushtakiwa.Reece jamesBeki Reece James atakua na nafasi ya kujibu tuhuma hizo mpaka kufikia Septemba 29 ndipo shirikisho litaamua kuchukua hatua dhidi ya beki huyo, Huku akikutwa hana hatia atafutiwa mashtaka lakini akikutwa na hatia ni wazi atafungiwa michezo kadhaa na kupigwa faini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.