YANGA YAPATA CHANGAMOTO ALGERIA

TAARIFA kutoka ndani ya Yanga kupitia kwa mjumbe wa kamati tendaji ya Yanga Alex Ngai amesema kuwa wamekutana na changamoto ya hali ya hewa tangu walipofika nchini humo.

Mbali na hilo Alex alisema, Yanga hawajafanya mazoezi yoyote hadi sasa kwa kuwa walipoteza mabegi yao ambayo yalikuwa na vifaa vingi vya wachezaji.yanga“Tangu tulivyofika juzi na Jana tumeshinda na mvua tu, mvua inanyesha asubuhi, mchana na usiku na baridi ni kali, hiyo ndio hali ya hewa ya huku ila haituondoi kwenye mipango yetu ya mchezo wa kesho.

“Pia kuna changamoto kubwa imetokea ambayo haipaswi kutokea kwa timu ya mpira, mizigo yetu yote ambayo tulikuja nayo ilibaki kwenye ndege jambo ambalo limetupa usumbufu mkubwa, hatujafanya mazoezi toka tumekuja huku.”Alisema Mjumbe huyo wa kamati tendaji ya Yanga

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.