Di Maria Copa America 2024 Itakua Mwisho Argentina

Winga wa klabu ya Benfica Angel Di Maria ameweka wazi kua michuano ya Copa America ambayo itachezwa mwaka 2024 ndio itakua mara ya mwisho wa yeye kuicheza timu ya taifa ya Argentina.

Angel Di Maria amekua akiitumikia timu ya taifa kwa muda mrefu ameeleza wazi baada ya kufanikiwa kushinda karibia kila taji na timu hiyo michuano ya Copa America ndio itakua ya mwisho ya kuitumikia timu hiyo.di mariaWinga Di Maria ameitumikia timu ya taifa ya Argentina tangu mwaka 2008 hivo ni takribani miaka 15 anaitumikia timu hiyo, Huku akifanikiwa kushinda mataji mawili makubwa Copa America mwaka 2021 na kombe la dunia mwaka 2022.

Winga huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid ameeleza kua amepambana kwa kiwango kikubwa kwa jasho na damu kwa timu hiyo, Hivo mwaka 2024 kwenye michuano ya Copa America itakua muda wa kusema kwaheri kwenye mchezo ambao amekua akiupenda.

Acha ujumbe