Winga wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Manchester United, PSG, na klabu ya Juventus Angel Di Maria ameamua kurejea kwenye klabu yake ya zamani klabu ya Benfica.
Angel Di Maria ambaye alikua anaitumikia klabu ya Juventus msimu uliomalizika akitokea klabu ya PSG winga huyo amecheza kwa kiwango bora ndani ya Juventus, Lakini hayupo tayari kuendelea kuwatumikia vibibi kizee hao wa Turin.Klabu ya Benfica inataka kumrejesha winga huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye amewahi kuitumikia klabu hiyo kwa ubora mkubwa kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2010 na wako katika hatua za mwisho.
Winga Angel Di Maria alikua anahitajika na klabu mbalimbali barani ulaya na hata nje ya bara ulaya, Lakini mchezaji huyo ameamua kuendelea kubaki ulaya na kurejea kwenye klabu ya Benfica ambayo ndio klabu yake ya kwanza barani ulaya.Angel Di Maria na klabu ya Benfica ni suala muda tu kwani wameshakubaliana pande zote mbili baina ya mchezaji na klabu, Kwani winga huyo ameonesha taa ya kijani kwa wababe hao wa soka nchini Ureno kua anataka kujiunga nao kwa mara nyingine.