Chelsea Waikataa Ofa ya United Tena Kwa Mount

Klabu ya Chelsea imekataa ofa ya klabu ya Manchester United kwa mara nyingine kwajili ya kumsajili kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount.

Chelsea walikataa ofa ya klabu ya Man United ya kiasi cha paundi milioni 40 mara ya kwanza lakini klabu hiyo imerudi tena na ofa ya puandi milioni 45 huku kukiwa na nyongeza ya puandi tano ili kufika paundi milioni 50 lakini klabu hiyo imegoma na wanataka paundi milioni 60. ChelseaManchester United wanamuwinda kiungo Mason Mount na yupo kwenye orodha ya juu kabisa katika wachezaji ambao wanawahitaji msimu huu, Lakini changamoto imekua ni kiasi cha pesa ambacho wamekieka Chelsea kwa mchezaji huyo.

Manchester United wanaripotiwa kutokuongeza ofa hiyo japo bado mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbele, Hivo lolote linaweza kutokea mbeleni na kuna uwezekano wakaongeza ofa au makubaliano yakabaki kwenye ofa hiyohiyo.ChelseaKlabu ya Chelsea mpaka sasa imekubali kumuuza kiungo wake Kai Havertz kwenda klabu ya Arsenal ambao wametoa ofa ambayo imekubalika kwa haraka, Huku Man United wao bado wakiwa hawajafikia ofa ambayo klabu hiyo inaihitaji.

Acha ujumbe