Azam Yamuongezea Mkataba Bajana

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kumuongezea mkataba kiungo wake matata klabuni hapo Sospeter Bajana ambaye ataendelea kusalia nda ni ya timu hiyo mpaka Juni 2026.

Azam wameachana na wachezaji wengi sana kwenye dirisha hili lakini pia inajaribu kukiimarisha kikosi chake kwa namna ya tofauti, Kwani wameanza kwa kuwaongezea mkataba wachezaji wake muhimu ndani ya klabu kabla ya kuanza kufanya sajili zingine nje ya klabu.AZAMMatajiri hao wa jiji la Dar-es-salaam wameahidi kuja kivingine msimu ujao kwani kwenye dirisha hili wamepitisha fagio kubwa sana ndani ya timu hiyo, Huku lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha klabu hiyo inafanya vizuri msimu ujao.

Klabu ya Azam imehakikisha inamfunga Bajana klabuni hapo baada ya kumuongezea  mkataba wa miaka mitatu, Kwani kulikua na tetesi za mchezaji huyo kutakiwa na wekundu wa msimbazi klabu ya Simba siku kadhaa nyuma.AZAMAzam inaelezwa baada ya Bajana kuongeza mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo wataendelea kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu ndani ya klabu hiyo ambao wanaona wanafaa kwenye timu hiyo kuelekea msimu ujao mwaka 2023/24.

Acha ujumbe