TAARIFA kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa kiungo wa klabu hiyo raia wa Burkinafaso Stephen Azizi KI ataendelea kubaki ndani ya klabu hiyo.
Makubaliano baina ya Uongozi wa Young Africans na kiungo wake Stephane Aziz Ki yalishafikiwa na Aziz Ki ataendelea kusalia Yanga kwa mara nyingine tena.
Huku taarifa zikidai muda wowote kuanzia sasa mchezaji huyo atatangazwa kuwa bado ni mali ya klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani na Twiga Kariakoo.
Hivi majuzi zilizaliwa taarifa kuwa nyota Aziz Ki huwenda akatimka kwenye klabu hiyo baada ya kupata kubwa nje ya Tanzania.

