KIUNGO wa Yanga Stephane Aziz Ki amefanikiwa kuibuka Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba wa Yanga SC, baada ya kuwashinda Dickson Job na Max Nzengeli.
Aziz Ki mwezi Oktoba ameisaidia timu yake kupata ushindi kwenye michezo mitatu, dhidi ya Geita Gold, Azam FC na Singida Fountain Gate FC.Kwenye michezo mitatu ya mwezi Oktoba amefunga mabao manne (4) ikiwemo Hat-Trick dhidi ya Azam FC, Azizi Ki amepata million nne (4) pamoja na tuzo.