Kocha Mkuu Yanga Sc Miguel Gamondi amesema kuwa kuelekea mchezo wa leo dhidi ya CR Belouzida watakwenda kucheza soka safi na la kuvutia sana.
Gamondi alisema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huwa siyo rahisi lakini wao wamejipanga vizuri na watapambana kupata matokeo wakiwa ugenini.
“Wananchi waendelee kuiamini timu yao na nina imani kesho tutacheza soka la kuburudisha na kupata matokeo ya kuridhisha.
“Tutajitahidi kucheza soka safi la kuvutia hata kama tupo ugenini,” alisema.
Yanga chini ya kocha Gamondi watacheza mechi yao ya kwanza leo dhidi ya CR Belouzidad ya nchini Algeria, mechi ikipigwa saa 4 usiku kwa saa za Tanzania

