GAMONDI KWENYE SURA MPYA DHIDI YA WAPINZANI

MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa anaingia uwanjani kulingana na aina ya wapinzani ambao atakutana nao ndani ya dakika 90.

Novemba 5 Yanga ilikomba pointi tatu mazima dhidi ya watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi.gamondiBaada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga. Pointi tatu kibindoni na kutibua rekodi ya Simba kucheza mechi saba za msimu wa 2023/24 bila kufungwa kuendelea.

Gamondi amesema kuwa wanatambua kwamba kazi kubwa kwenye mechi zao zote ni kusaka ushindi wakibadili mbinu kulingana na mchezo husika.

“Kila mchezo unakuja kulingana na aina ya wapinzani ambao tunakutana nao. Tunatambua namna ushindani ulivyo hilo lipo wazi hivyo tunaingia uwanjani tukiwa na mpango kazi wa kusaka ushindi.gamondi“Kikubwa ni kuona kwamba tunacheza vizuri na kuwapa burudani mashabiki wetu ambao wanajitokeza uwanjani. Wazidi kuwa pamoja nasi kazi bado ipo na tunaamini tutafanya vizuri,” amesema Gamondi.

Acha ujumbe