Klabu ya Fiorentina imethibitisha kumsajili beki wa pembeni Tariq Lamptey kwa uhamisho wa kudumu akitokea Brighton & Hove Albion.

Kwa mujibu wa taarifa, mtaalamu wa usajili wa Football Italia, Alfredo Pedullà, aliripoti kwa kipekee kwamba Fiorentina na Brighton walifikia makubaliano siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana amekamilisha uhamisho wa thamani ya €6 milioni pamoja na nyongeza kadhaa (add-ons).
Lamptey alizaliwa Hillingdon, England, Septemba 30, mwaka 2000. Alipitia kwenye mfumo wa vijana wa Chelsea kabla ya kuhamia Brighton, ambapo katika misimu mitano iliyopita amecheza mechi 122 kwenye Premier League, Europa League, FA Cup na EFL Cup, akifunga magoli matano na kutoa pasi 12 za mabao.


