Klabu ya Tabora United, iliyokuwa ikiwakilisha mkoa wa Tabora katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, sasa imeingia katika sura mpya baada ya kununuliwa rasmi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kwa mabadiliko haya, jina la klabu limebadilishwa na sasa itajulikana kama TRA United SC.
Hatua hii pia imeambatana na uhamisho wa makazi ya klabu hiyo kutoka Tabora hadi jijini Dar es Salaam, jambo linaloifanya Dar es Salaam kuwa na jumla ya timu sita zinazoshiriki Ligi Kuu. TRA United SC inaungana na vigogo Simba SC, Yanga SC, Azam FC, KMC FC na JKT Tanzania katika kuwakilisha jiji hilo kwenye medani ya soka la ushindani.


