Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, anakabiliwa na presha kubwa baada ya kikosi chake kushuka hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Premier League kufuatia kipigo cha 3-1 dhidi ya Brentford. Licha ya ushindi wa morali dhidi ya Chelsea siku chache kabla, United walionekana kupoteza mwelekeo kabisa kwenye uwanja wa Gtech Community Stadium.
Benjamin Sesko alifunga bao lake la kwanza akiwa na United, lakini juhudi zake ziligubikwa na udhaifu wa kikosi kilichoruhusu mabao mawili ndani ya dakika 20 za kwanza, na cha tatu katika dakika za majeruhi. Matokeo hayo yamewaacha mashabiki wakihofia kurejea kwa hali ya msimu uliopita, kutokuwa na mwelekeo, kukosa ubunifu, na matokeo yasiyoridhisha.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Goal na Sports Mole, Manchester United wanatazama kwa makini tarehe 1 Novemba, ambapo fidia ya kumfuta kazi Amorim itapungua kwa kiasi kikubwa. Hii imezua tetesi kuwa klabu inaweza kusubiri hadi tarehe hiyo kabla ya kufanya maamuzi rasmi.
Sir Jim Ratcliffe, mmiliki mwenza wa United kupitia kampuni ya INEOS, anaripotiwa kuwa na nia ya kumleta Gareth Southgate kama kocha mpya. Southgate, ambaye aliongoza England kufika fainali za Euro 2020 na Euro 2024, yuko huru tangu alipojiuzulu baada ya mashindano ya Ulaya mwaka huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.



