Klabu ya Simba ipo kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kutupa karata yao ya kwanza wakiwa ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatin, huku nyota wawili raia wa Afrika Kusini, Neo Maema na De De Reuck wakipewa jukumu nzito.
Neo Maema na De De Reuck wamepewa jukumu la kupambana zaidi kwa kuwa wanawafahamu vema Nsingizini Hotspurs kutokana na ujirani na wameshakutana mara kadhaa kwenye mashindano ya Cosafa.
Simba watashuka dimbani kesho saa 10 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki na utakuwa mchezo wa kwanza kwenye hatua ya pili ya kusaka nafasi ya kutinga katika hatua ya makundi.
Hii ni kete ya kwanza kimataifa kwa Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev huku wachezaji wapya wa timu hiyo ikiwa ni Neo Maema, De Reuck wakipewa angalizo kuhakikisha kwamba wanapambana kupata matokeo mazuri.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Ikumbukwe kwamba mshindi wa jumla katika mchezo huu atakwenda hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amebainisha kuwa wachezaji wote wana kazi kuelekea mchezo ujao kimataifa kuhakikisha wanaendeleza utamaduni wa timu hiyo kupata matokeo mazuri.
“Wachezaji wapya baadhi De Reuck na Neo Maema wanaifahamu historia waliyoikuta Simba ya ushiriki wetu wa kimataifa na siyo hao pekee pia wachezaji wengine kama yupo hafahamu umuhimu wa kufuzu makundi lazima atambue na kuendeleza ile historia,”
Mchezo wa Nsingizini Hotspurs vs Simba SC ni Oktoba 19 2025 na ule wa marudiano ni Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, kwenye CAF Champions League.