Singida Black Stars Yafafanua Tuhuma Dhidi ya Kipa wao Amas Obasogie

Klabu ya Singida Black Stars imetoa ufafanuzi kuhusu wasiwasi uliokuwa umeibuka miongoni mwa viongozi, mashabiki na wadau wa soka kufuatia makosa ya kujirudia katika baadhi ya michezo ya hivi karibuni ya timu hiyo yaliyo asabishwa na kipa wao rai awa Nigeria, Amasi Obasogie hali iliyosababisha kuhisi kuwa anapanga matokeo.

Singida Black Stars Yafafanua Tuhuma Dhidi ya Kipa wao Amas Obasogie

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, wasiwasi huo ulitokana na matokeo ya michezo iliyochezwa dhidi ya Flambeau du Centre katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na michezo ya ligi kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji fc na Namungo fc.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kutokana na hali hiyo, menejimenti ya klabu kupitia kamati ya nidhamu ilianzisha uchunguzi wa awali kuhusiana na taarifa za wasiwasi zilizomhusu kipa wa timu hiyo, Amas Obasogie.

Singida Black Stars Yafafanua Tuhuma Dhidi ya Kipa wao Amas Obasogie

Baada ya kufanya uchunguzi pamoja na maelezo ya mchezaji na taarifa za uhakika kutoka kwa Meneja Mkuu wa klabu, ilibainika kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa upangaji wa matokeo au mchezo wa bahati nasibu. Klabu imeeleza kuwa makosa yaliyoonekana yalitokana na changamoto za kiufundi zilizotokea ndani ya mchezo.

Hata hivyo, Obasogie ameomba radhi kwa tukio lililosababisha tafsiri tofauti miongoni mwa mashabiki na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Kutokana na matokeo ya uchunguzi huo, klabu imeamua kutengua uamuzi wa awali wa kumsimamisha kwa miezi mitatu na kumruhusu kuendelea na majukumu yake kikosini.

Singida Black Stars Yafafanua Tuhuma Dhidi ya Kipa wao Amas Obasogie

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.