Mchezaji wa zamani wa Yanga SC ambaye kwa sasa ni kocha na mchambuzi wa soka, Ally Mayay Tembele, amesema anaamini kwamba winga wa Simba SC, Libasse Gueye, ni mchezaji mzuri lakini bado hajaonesha ubora wake wote uwanjani.

Mayay ameeleza kuwa Gueye ana uwezo mkubwa wa kucheza katika safu ya ushambuliaji na anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Simba ikiwa ataendelea kupewa nafasi zaidi ya kuonyesha kipaji chake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Libasse Gueye ni moja kati ya wachezaji ambao wana uwezo mkubwa sana hususan katika eneo la ushambuliaji. Ni mchezaji ambaye anategemewa kuanzisha mashambulizi, kumalizia na pia ana uwezo wa kulazimisha mabeki wengi kufanya makosa kutokana na kasi yake na uwezo alionao.” Amesema Ally Mayai
Aidha, Mayay ameongeza kuwa endapo Gueye atapewa nafasi za kutosha na kuonyesha uthubutu katika uchezaji wake, anaweza kufanya mambo makubwa na kuwa muhimu sana kwa timu katika mashindano ya ligi na michuano mingine.


