Joan Laporta Alikataa Lionel Messi Kurudi FC Barcelona

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa FC Barcelona, Xavi Hernández, amefichua kuwa kulikuwa na mpango uliokaribia kukamilika wa kumrejesha nyota wa soka Lionel Messi katika klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa kombe la Dunia 2022 aliyoshinda akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

Joan Laporta Alikataa Lionel Messi Kurudi FC Barcelona

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la La Vanguardia, Xavi alisema kuwa mchakato wa kumrudisha Messi ulikuwa umefikia hatua nzuri na hata upande wa LaLiga ulikuwa tayari umetoa ruhusa ya awali kwa mpango huo kutekelezwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Xavi alieleza kuwa Messi mwenyewe alikuwa na nia ya kurejea FC Barcelona, klabu ambayo aliitumikia kwa mafanikio makubwa kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya kuondoka mwaka 2021. Hata hivyo, licha ya mambo mengi kuonekana kwenda sawa, mpango huo haukuweza kukamilika.

Joan Laporta Alikataa Lionel Messi Kurudi FC Barcelona

Kwa mujibu wa Xavi, Rais wa Barcelona Joan Laporta ndiye aliyesimamisha usajili huo akieleza kuwa kurejea kwa Messi kungeweza kuibua changamoto ya mishahara ndani ya kikosi, hali ambayo klabu isingeweza kuimudu kifedha wakati huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.