Pepe Aiokoa Villarreal Dakika za Mwisho Dhidi ya Alaves

Klabu ya Villarreal CF imepata sare ya 1-1 dhidi ya Deportivo Alavés katika mchezo wa La Liga, baada ya mshambuliaji Nicolas Pépé kufunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho kabisa za mchezo.

Pepe Aiokoa Villarreal Dakika za Mwisho Dhidi ya AlavesMchezo huo ulikuwa wa kwanza wa nyumbani kwa kocha Quique Sánchez Flores tangu achukue mikoba ya kuinoa Alaves, akikutana na Villarreal iliyo chini ya kocha Marcelino García Toral. Kipindi cha kwanza kilikuwa na ushindani mdogo huku Villarreal wakishindwa kutumia nafasi dhidi ya wapinzani wao waliopo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alaves walipata bao la kuongoza dakika ya 40 baada ya shambulizi lililoanzia kwa Toni Martínez, aliyetoa pasi ya kisigino ndani ya eneo la hatari kabla ya beki Rafa Marín kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira.

Pepe Aiokoa Villarreal Dakika za Mwisho Dhidi ya AlavesKipindi cha pili kilishuhudia mchezo ukiwa mgumu zaidi kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha mjini Vitoria-Gasteiz, huku timu zote zikishindwa kutumia ipasavyo nafasi walizopata. Villarreal walijaribu kusawazisha kupitia mashambulizi ya Pépé na Georges Mikautadze, lakini kipa Antonio Sivera aliendelea kuokoa hatari.

Hata hivyo, wakati Alaves wakiamini wangeshinda mchezo huo, Pépé aliibuka shujaa kwa Villarreal baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 98 kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililompita kipa Sivera na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Pepe Aiokoa Villarreal Dakika za Mwisho Dhidi ya AlavesMatokeo hayo yanaiacha Alaves bila ushindi katika michezo sita ya ligi mfululizo, huku Villarreal nao wakiongeza presha baada ya kushinda mchezo mmoja tu katika michezo yao sita ya ugenini kwenye La Liga.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.