Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayer Leverkusen mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano, na kushinda kwa jumla ya mabao 3-1.
Arsenal ilianza mchezo huo kwa kasi kubwa ikitengeneza nafasi kadhaa kupitia Leandro Trossard, lakini juhudi zake ziliishia kuzuiwa na kipa wa Leverkusen Janis Blaswich ambaye alikuwa imara langoni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao la kwanza lilipatikana kupitia Eberechi Eze aliyefunga kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari, likiwa bao lake la kwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal waliendelea kuimarisha ushindi wao pale Declan Rice alipoongeza bao la pili kwa shuti la kuvutia lililojaa ustadi mkubwa kutoka nje ya boksi.
Licha ya Leverkusen kujaribu kusawazisha, walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Arsenal huku kipa David Raya akifanya kazi nzuri kuokoa michomo michache iliyolenga lango.
Ushindi huo unaifanya Arsenal kusonga mbele na sasa watakutana na Sporting CP katika robo fainali, huku Leverkusen wakielekeza nguvu zao kwenye kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao.

