Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris Saint Germain, wameivunja moyo Chelsea baada ya kuichapa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Stamford Bridge, na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-2.
Chelsea waliingia uwanjani wakiwa na matumaini ya kufanya comeback ya kihistoria, lakini ndoto zao zilianza kufifia mapema baada ya Khvicha Kvaratskhelia kufunga bao la mapema kufuatia makosa ya safu ya ulinzi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
PSG waliendeleza presha na kuongeza bao la pili kupitia Bradley Barcola, akimalizia shambulizi la kushtukiza baada ya Chelsea kupoteza mpira katikati ya uwanja.
Licha ya juhudi za Chelsea kurejea mchezoni, walikwama mbele ya kipa Matvei Safonov ambaye aliokoa michomo kadhaa hatari kutoka kwa João Pedro na Cole Palmer.
Kipindi cha pili, PSG walithibitisha ubora wao baada ya Senny Mayulu kufunga bao la tatu, akimalizia shambulizi jingine la kushtukiza na kuzima kabisa matumaini ya Chelsea.
Matokeo hayo yameifanya PSG kusonga mbele hadi robo fainali huku wakiendelea na rekodi nzuri dhidi ya timu za England, wakati Chelsea wakizidi kuporomoka kwa matokeo mabaya pamoja na kuandamwa na majeraha ya wachezaji wao.

