O’Reilly Ang’ara Man City Ikitwaa Ubingwa wa Carabao kwa Kuichapa Arsenal 2-0

Nyota chipukizi Nico O’Reilly alifunga mabao mawili kipindi cha pili na kuisaidia Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika fainali ya Kombe la Carabao (EFL Cup).

O’Reilly Ang’ara Man City Ikitwaa Ubingwa wa Carabao kwa Kuichapa Arsenal 2-0Arsenal walionekana kuanza mchezo kwa nguvu wakitengeneza nafasi kadhaa kupitia Kai Havertz na Bukayo Saka, lakini juhudi zao zilikwama baada ya kipa James Trafford kuokoa hatari tatu mfululizo na kuinyima mabao ya mapema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kadri mchezo ulivyoendelea, Manchester City walizidi kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kupitia Antoine Semenyo na Erling Haaland, lakini safu ya ulinzi ya Arsenal iliendelea kuwa imara hadi mapumziko.

O’Reilly Ang’ara Man City Ikitwaa Ubingwa wa Carabao kwa Kuichapa Arsenal 2-0Kipindi cha pili kilianza kwa presha kubwa kutoka kwa City, na hatimaye walipata bao la kuongoza dakika ya 60 baada ya krosi ya Rayan Cherki kumpita kipa Kepa Arrizabalaga na kumkuta O’Reilly aliyefunga kwa kichwa ndani ya eneo la hatari.

Dakika nne baadaye, O’Reilly aliongeza bao la pili kwa kichwa kingine safi kufuatia krosi ya Matheus Nunes, akiiweka City katika nafasi nzuri ya kushinda mchezo huo. Licha ya juhudi za Mikel Arteta kufanya mabadiliko, Arsenal walishindwa kurejea mchezoni.

O’Reilly Ang’ara Man City Ikitwaa Ubingwa wa Carabao kwa Kuichapa Arsenal 2-0Akizungumza baada ya ushindi huo, kocha wa City Pep Guardiola alisema “Tulionyesha ubora na subira hadi tukapata mabao yetu. Ni ushindi mkubwa kwa timu na mashabiki wetu.”

O’Reilly Ang’ara Man City Ikitwaa Ubingwa wa Carabao kwa Kuichapa Arsenal 2-0Kwa upande wake Arteta alisema “Tulianza vizuri lakini hatukutumia nafasi zetu. Makosa madogo yametuadhibu na kutugharimu taji.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.