Nahodha wa West Ham United, Jarrod Bowen, amewataka wachezaji wenzake kubaki wamoja na kupambana hadi mwisho huku vita ya kuepuka kushuka daraja ikizidi kuwa ngumu baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya Aston Villa Jumapili katika Premier League.
Mabao yaliyofungwa na John McGinn na Ollie Watkins kabla na baada ya mapumziko yaliipa Aston Villa ushindi muhimu unaoimarisha matumaini yao ya kufuzu UEFA Champions League, huku West Ham wakibaki katika nafasi ya 18 wakiwa na pointi 29 baada ya mechi 31.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mapambano ya kushuka daraja, hali imezidi kuwa mbaya kwa baadhi ya timu nyingine, huku Tottenham Hotspur walio nafasi ya 17 wakipokea kichapo cha mabao 3-0 nyumbani kutoka kwa Nottingham Forest.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Bowen alisema “Bila kujali matokeo ya leo, tunapaswa kujikita kwenye sisi wenyewe. Tunahitaji kurejea kwa nguvu baada ya mapumziko na kumaliza msimu vizuri. Ukweli ni kwamba walikuwa bora kuliko sisi leo, jambo ambalo ni gumu kulikubali.”
Bowen aliongeza “Bado tunaamini tuko katika nafasi nzuri, hatupaswi kuruhusu matokeo haya kufuta juhudi zetu zote. Haukuwa msimu mzuri kwetu, lakini lazima tuendelee kupambana ili kubaki kwenye ligi.”
Kwa upande wa Aston Villa, kocha Unai Emery alimpongeza Watkins akisema “Yeye ni mpiganaji na anatekeleza majukumu yake kila wakati. Leo amefunga, lakini anatakiwa kuwa na uthabiti zaidi ili kuongeza takwimu zake na kumpa kocha wa taifa changamoto ya kumchagua.”

