Saltor: Spurs Washindwa Kubebeka na Presha ya Vita YA Kushuka Daraja

Kocha msaidizi wa Tottenham Hotspur, Bruno Saltor, amekiri kuwa timu yake ilishindwa kukabiliana na presha ya mchezo muhimu wa kupambana na kushuka daraja baada ya kufungwa mabao 3-0 na Nottingham Forest Jumapili.

Saltor: Spurs Washindwa Kubebeka na Presha ya Vita YA Kushuka DarajaKipigo hicho kimeiacha Spurs ikiwa na tofauti ya pointi moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja katika Premier League, hali inayoongeza wasiwasi kwa mashabiki na uongozi wa klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Saltor alisimamia mkutano na waandishi wa habari kwa niaba ya kocha mkuu Igor Tudor ambaye alikuwa anashughulikia msiba wa kifamilia. Licha ya matokeo mabaya, alisema kulikuwa na dalili chanya katika mechi mbili zilizopita pamoja na kiwango cha kipindi cha kwanza dhidi ya Forest.

Saltor: Spurs Washindwa Kubebeka na Presha ya Vita YA Kushuka DarajaHata hivyo, alikiri kuwa timu ilipoteza mwelekeo kipindi cha pili na kushindwa kuhimili uzito wa mchezo huo muhimu, jambo lililosababisha kuporomoka kwa kiwango na kuruhusu mabao ya haraka.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Saltor alisema “Unaweza kuona wachezaji wanajali na wanajitahidi kwa asilimia 100, lakini kwa sasa haitoshi. Tunahitaji kupunguza makosa kwa sababu tunajua tutaruhusu mabao.”

Saltor: Spurs Washindwa Kubebeka na Presha ya Vita YA Kushuka DarajaAliongeza “Dakika 44 za kwanza zilikuwa nzuri sana, lakini kipindi cha pili hatukuweza kubeba uzito wa mchezo. Kwa sasa, sote tuna lengo moja kupambana hadi mwisho wa msimu na kubaki kwenye ligi kama klabu hii inavyostahili

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.