Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Galatasaray, Victor Osimhen, amefanyiwa upasuaji kufuatia kuvunjika mkono wake wa kulia, klabu hiyo imethibitisha rasmi.
Osimhen alipata jeraha hilo wakati wa mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Liverpool uliopigwa katika dimba la Anfield, ambapo alilazimika kutolewa kipindi cha mapumziko baada ya madaktari kubaini uvimbe mkubwa mkononi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia taarifa yao, Galatasaray wamesema “Mchezaji wetu Victor Osimhen, ambaye alipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo wetu wa ugenini dhidi ya Liverpool katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, amefanyiwa upasuaji uliofanikiwa leo katika Hospitali ya Maslak Acıbadem, chini ya usimamizi wa daktari wa klabu, Op. Dr Yener Ince. Tunamtakia kila la heri na tunatarajia arejee uwanjani haraka iwezekanavyo.”
Daktari wa klabu hiyo, Yener Ince, aliongeza kuwa maendeleo ya mchezaji huyo yatafuatiliwa kila siku huku akisema “Amefanyiwa upasuaji wa mafanikio. Timu ya madaktari itafanya kila linalowezekana kuhakikisha anarudi uwanjani haraka, na taarifa zaidi zitatolewa kadri mchakato unavyoendelea.”
Ingawa tarehe rasmi ya kurejea haijawekwa wazi, Osimhen mwenyewe alieleza kupitia mahojiano ya mtandaoni kuwa anaweza kurejea ndani ya wiki tano hadi sita, akisema “Itachukua muda usiozidi wiki sita. Mara nyingi ni wiki nne za kupona, kisha wiki mbili za mazoezi binafsi kabla ya kurejea kikosini.”
Nyota huyo wa zamani wa Lille na Napoli, ambaye tayari amefunga mabao 19 katika mechi 29 msimu huu, anatarajiwa kuukosa mchezo muhimu wa ligi dhidi ya Fenerbahçe Aprili 26.

