Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Gennaro Gattuso, amesema kuwa mchezo wa nusu fainali ya mtoano wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Northern Ireland ndio muhimu zaidi katika maisha yake ya ukocha.
Italia itawakaribisha wapinzani wao katika mji wa Bergamo huku wakisaka kurejea kwenye michuano hiyo baada ya kukosa fainali mbili zilizopita.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Gattuso alinukuliwa akisema “Kesho ni mechi muhimu zaidi katika maisha yangu ya ukocha. Nipo tayari, sitaki kufikiria mabaya bali nataka kufikiri makubwa na tutapambana kwa nguvu zote.” Kauli hiyo inaonesha presha kubwa iliyopo kwa Italia ambayo haijacheza hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia tangu ilipotwaa taji mwaka 2006.
Kocha huyo pia alikiri kuwa mchezo huo una uzito mkubwa hata kuliko fainali ya Kombe la Dunia ya mwaka 2006 aliyoshinda akiwa mchezaji dhidi ya Ufaransa. Aidha, alitania kuwa presha ya mchezo huo humfanya ashindwe kulala, akisema wakati mwingine hulazimika kutumia dawa za usingizi.
Kwa upande wa kikosi, Gattuso alibainisha kuwa wachezaji wengi wako fiti isipokuwa mabeki wachache wenye mashaka ya kucheza akiwemo Alessandro Bastoni pamoja na mshambuliaji Gianluca Scamacca. Hali hiyo inatoa matumaini kwa Italia kuelekea mchezo huo muhimu.
Naye mshambuliaji Mateo Retegui amesema timu imejipanga kuhakikisha inashinda, akisisitiza kuwa hakuna matokeo mengine wanayoyahitaji zaidi ya ushindi. “Tunapaswa kuwa watulivu na kucheza bila presha kubwa, lakini tunajua ushindi pekee ndio chaguo letu,” alisema.
Kwa upande wa kocha wa Ireland Kaskazini, Michael O’Neill, amesema hawapaswi kuogopa ukubwa wa Italia bali wanahitaji kuifanya mechi kuwa ngumu. “Tunaiheshimu Italia, lakini tunahitaji kucheza kwa nidhamu na kuwapa wakati mgumu. Presha ipo kwao zaidi kutokana na historia yao,” alisisitiza.

