Kocha mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema timu yake inalenga kufikia hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA kwa mara ya nane mfululizo watakapokutana na Liverpool FC leo Jumamosi.
Guardiola alisema mafanikio hayo yatakuwa ya kipekee na ya kihistoria, huku akisisitiza umuhimu wa mashindano hayo: “Kesho tuna nafasi ya kufikia hatua ya ajabu, kucheza nusu fainali mara nane mfululizo. Hili halijawahi kutokea… ni mashindano yenye hadhi kubwa na yenye ushindani mkali, hasa ukizingatia mpinzani wetu ni Liverpool.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
City inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali ya juu baada ya kushinda Kombe la Ligi kwa kuifunga Arsenal FC kabla ya mapumziko ya kimataifa, huku Guardiola akitarajia timu yake kuendeleza ubora huo katika harakati za kutwaa mataji zaidi msimu huu.
Licha ya mafanikio makubwa aliyopata tangu ajiunge na City mwaka 2016, Guardiola alikiri kuwa Liverpool imekuwa mpinzani mgumu kwake “Mara nyingi wamekuwa wapinzani wetu wakubwa… wana wachezaji wa kiwango cha juu sana. Tunahitaji kucheza katika kiwango kile kile tulichoonyesha dhidi ya Arsenal ili kufikia hatua inayofuata.”
Kocha huyo pia alimpongeza mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, ambaye ametangaza kuondoka mwishoni mwa msimu: “Bila shaka ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa. Takwimu zake na uthabiti wake ni wa kipekee… ni gwiji wa Liverpool na pia wa Ligi Kuu.”
Hata hivyo, Guardiola alikwepa kuzungumzia mustakabali wa kiungo wake Rodri, ambaye amehusishwa na kuhamia Real Madrid, akisema: “Sina uhakika, sina maoni… najua nia ya klabu na labda yake pia, lakini siwezi kusema zaidi.”

