Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limetangaza orodha ya waamuzi watakaochezesha mechi za Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, likiwajumuisha jumla ya waamuzi 52, wakiwemo wanawake sita.
Mbali na waamuzi hao wa kati, FIFA pia imeteua waamuzi wasaidizi 88 pamoja na maafisa 30 wa VAR (Video Assistant Referee), wote wakitoka katika mashirikisho sita ya soka duniani na nchi wanachama 50.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mkuu wa idara ya waamuzi wa FIFA, Pierluigi Collina, amesema waamuzi walioteuliwa ni miongoni mwa bora zaidi duniani, wakichaguliwa baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka mitatu.
“Waamuzi walioteuliwa ni bora zaidi duniani. Walikuwa sehemu ya kundi kubwa lililotambuliwa na kufuatiliwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wamehudhuria semina na kuchezesha mashindano mbalimbali ya FIFA,” amesema Pierluigi Collina.
Ameongeza kuwa, “Mbali na hilo, viwango vyao vimekuwa vikifanyiwa tathmini mara kwa mara kupitia mechi za ndani na za kimataifa ili kuhakikisha ubora wao unaendelea kuimarika.”
Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika katika nchi za United States, Canada na Mexico linatarajiwa kuwa kubwa zaidi katika historia, likihusisha timu 48 na jumla ya mechi 104, ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na mashindano ya 2022 FIFA World Cup yaliyokuwa na timu 32 na mechi 64.
Kwa upande wa ushiriki wa wanawake, Pierluigi Collina amesema “Uteuzi wa waamuzi sita wanawake unaendeleza mwelekeo ulioanza miaka minne iliyopita huko Qatar, ambapo pia wanawake walipata nafasi ya kuchezesha mechi za Kombe la Dunia.”

