Klabu ya Real Madrid inatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika dirisha la usajili la majira ya joto 2026, ambapo jumla ya wachezaji saba wanatarajiwa kuondoka ili kupisha sura mpya kikosini. Hatua hii inaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa kuijenga upya timu kwa ushindani wa hali ya juu barani Ulaya.
Katika orodha ya wanaotarajiwa kuuzwa, majina kama Eduardo Camavinga, Dani Ceballos, Raúl Asencio pamoja na Gonzalo García yamejitokeza. Uamuzi huu unaashiria mabadiliko ya kiufundi yanayolenga kuboresha kikosi kwa muda mrefu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Wakati huo huo, beki mkongwe David Alaba na nahodha Dani Carvajal wanatarajiwa kuondoka kama wachezaji huru baada ya mikataba yao kumalizika, huku kijana Franco Mastantuono akipangwa kutolewa kwa mkopo ili kupata uzoefu zaidi wa kucheza.
Ili kuziba mapengo hayo, Real Madrid imepanga kufanya usajili mkubwa wa wachezaji wapya. Beki wa Liverpool, Ibrahima Konaté, anatajwa kuwa miongoni mwa wanaonyatiwa kusajiliwa kama mchezaji huru.
Majina mengine makubwa yanayotajwa kujiunga na Real madrid ni pamoja na Vitinha kutoka Paris Saint-Germain, Adam Wharton wa Crystal Palace, pamoja na Rodri wa Manchester City, ambao wanatarajiwa kuimarisha safu ya kiungo kufuatia pengo lililoachwa na Toni Kroos.
Aidha, chipukizi Nico Paz anatarajiwa kurejeshwa kikosini ili kuongeza nguvu mpya. Mabadiliko haya yanaashiria mwanzo wa enzi mpya ndani ya Real Madrid, huku mashabiki wakisubiri kuona matokeo ya mkakati huu mkubwa.

