Klabu kubwa ya Uturuki Fenerbahçe S.K. imemtimua kocha mkuu Domenico Tedesco kufuatia kipigo kizito cha dabi dhidi ya Galatasaray S.K..
Uamuzi huo umetangazwa Jumatatu, saa 24 baada ya Fenerbahce kupoteza kwa mabao 3-0 ugenini dhidi ya wapinzani wao wakuu, matokeo yaliyoathiri vibaya matumaini yao ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki (Super Lig).
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Tedesco, aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Belgium, alichukua nafasi ya José Mourinho mwezi Septemba lakini ameshindwa kumaliza msimu baada ya matokeo yasiyoridhisha.
Katika taarifa rasmi, klabu hiyo ilisema, “Tumefikia uamuzi wa kusitisha mkataba wa kocha wetu Domenico Tedesco pamoja na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi kufuatia matokeo ya hivi karibuni.”
Mchezo huo uliokuwa na mvutano mkubwa ulimshuhudia kiungo Anderson Talisca akikosa penalti kipindi cha kwanza, huku kipa Ederson Moraes akionyeshwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Fenerbahce sasa wako alama saba nyuma ya vinara Galatasaray S.K. wakiwa na mechi tatu pekee zilizobaki, huku kocha msaidizi Zeki Murat Göle akiteuliwa kuiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

