Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, amemsifu mshambuliaji wake Harry Kane akisema anaendelea kuwa bora kadri anavyozeeka, kuelekea nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Paris Saint-Germain.
Kane amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu, akifunga mabao 12 katika mechi 11 za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwemo mabao muhimu dhidi ya Real Madrid kwenye hatua ya robo fainali.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa ujumla, nyota huyo ameifungia Bayern mabao 53 katika mechi 45 msimu huu, takwimu zinazovutia hasa ukizingatia kuwa anakaribia kutimiza miaka 33 mwezi Julai.
Akizungumzia ubora wa Kane, Kompany alisema, “Amekuwa mshambuliaji wa kipekee mwenye uwezo wa kufunga kwa njia mbalimbali kwa kichwa, mguu wa kushoto, kulia na hata mashuti ya mbali.”
Aliongeza, “Kinachovutia zaidi sasa ni uwezo wake wa kusaidia timu, pasi zake, bidii na akili yake ya mchezo. Ameunganisha ubora huo na takwimu kubwa, jambo ambalo si rahisi.”
Bayern wanakabiliwa na PSG katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali, huku Kompany akisisitiza kuwa mechi kati ya timu hizo huwa na ushindani mkubwa, akisema, “Kila mara tunapokutana na PSG, mechi huwa ngumu sana na huamuliwa kwa maelezo madogo madogo.”

