Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewataka wachezaji wake kurejea kwenye malengo yao ya ubingwa wa Premier League wanapojiandaa kuikaribisha Fulham siku ya Jumamosi. Hii inakuja siku chache baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal wanaendelea kupambana kumaliza ukame wa zaidi ya miaka 20 bila ubingwa wa ligi, tangu mafanikio yao ya kihistoria ya msimu wa 2003/04 waliomaliza bila kufungwa “Tunahitaji kuangazia Fulham. Njaa ya kucheza, kushindana, kushinda na kusogea karibu na ndoto yetu,” alisema Arteta.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo alisisitiza wazi kuwa lengo lao kuu ni kutwaa ubingwa msimu huu huku wakielekea mwisho wa ligi. “Tunacheza kushinda Premier League. Hapo ndipo tulipotaka kuwa. Zimebaki mechi nne, tuko tayari kupambana,” aliongeza.
Licha ya kuongoza ligi kwa muda mrefu, Arteta alikiri kuwa kupoteza pointi mara kwa mara kumeipa nafasi Manchester City kusogea karibu, huku kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola kikiendelea kushinda mechi zake za mwisho wa msimu. “Zimebaki mechi nne tu na kila kitu kiko hatarini, hakuna wakati mzuri zaidi ya huu,” alisema.
Arteta pia alithibitisha kuwa mshambuliaji Kai Havertz na beki Jurrien Timber watakosekana katika mchezo dhidi ya Fulham kutokana na majeraha. Havertz aliumia katika mechi dhidi ya Newcastle United, huku Timber akiwa nje tangu Machi.
Hata hivyo, Arteta alitoa matumaini ya kurejea kwa Havertz katika mchezo wa marudiano dhidi ya Atletico Madrid.
“Amekuwa pengo kubwa kwetu. Ni mmoja wa wachezaji muhimu sana kwenye ushambuliaji. Hataweza kucheza mechi hii, lakini tunatarajia atakuwa tayari kwa Atletico. Anafanya kila jitihada kurejea haraka,” alihitimisha.

