Kama ilivyo kawaida wanasema mwenye bahati zake ametua ndani ya Italia na uwezo wake wote. Imekuwa kawaida sasa hivi kwa wababe wa vikombe ndani ya taifa hilo kushinda mechi zao mara nyingi na mara kwa mara kutokana na uwezo walionao kwa sasa ndani ya kikosi chao. Bado wanaendelea kushikilia ligi hiyo ya Serie A kwa sasa wakiwa na tofauti kubwa ya alama kutoka nafasi yao na yule anayewafuatia.
Juventus wamekuwa na mfuatano mzuri wa matokeo katika mechi zao zote za hivi karibuni hususan kwenye ligi hiyo ambayo wanaendelea kupigilia msumari wa alama kujiwekea nafasi nzuri ya kushinda michuano hiyo tena kwa msimu mwingine. Na wamekuwa wakichukua vikombe vingi sana hadi sasa.
Mara kadhaa Juve anapokutana na Napoli hushuhudiwa soka zuri la kuvutia lenye tambo za kila aina kati ya wawili hao; kutokana na timu zote mbili kuwa na historia kubwa ndani ya taifa hilo. Katika mechi waliyoicheza jana mengi yalitokea katika mtanange huo ambao mwenyeji wa mchezo huo aliweza kupoteza mechi yake kwa kufungwa 1-2.
Mtanange
Alikuwa ni Pjanic aliyewapa uongozi baada ya kucheza mpira uliomshinda mlinda mlango wa Napoli, Meret ambaye alionekana kuisaidia timu yake hiyo kutokupata kipigo cha aibu akiwa mbele ya mashabiki zake. Mechi ilizidi kupendeza kutokana na kila mmoja kutafuta njia ya kupata matokeo safi yenye kuvutia ili aweze kusonga mbele zaidi.
Hata kabla ya mapumziko Emre Can alipata nafasi murua ambayo aliweza kuzamisha shuti lenye ufundi na kumwacha mlinda mlango na walinzi wake wakiwa hawana la kufanya kabisa. Baada ya hapo zikashuhudiwa kadi ambazo ziliwafanya wachezaji waache kucheza kwa wakati fulani ili kupisha waliokosa nidhamu ya mchezo kujadiliana maamuzi na mwamuzi.
Ikashuhudiwa ndani ya mechi hiyo wachezaji wawili kupata kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu. Huku upande wa Napoli mlinda mlango akifanya kosa mbele ya Ronaldo na kupata kadi nyekundu ambayo ikamlazimu kutoka nje ya mechi hiyo ili kutumikia adhabu yake ya kinidhamu.
Yajayo
Baada ya ushindi huo sasa, Juve anajiandaa kukutana na Udinese ambao wamekuwa na matokeo mazuri wakati mwingine wanapocheza na wakubwa. Na kwao hicho ni kibarua kuangalia kama watajikita sana kutokana na alama walizonazo kwa sasa. Baada ya safari hiyo pia atakuwa na kazi ya kulipa kisasi mbele ya Atletico Madrid ambao waliweza kumfunga katika mechi iliyokuwa ya kuviziana sana.
Msimu huu wanaweza kufanya maajabu ndani ya taifa hilo kutokana na uwezo walionao, kikosi chao kipana na kuwa na wachezaji wenye uzoefu wa muda mrefu ndani ya kikosi hicho. Hawana cha kupoteza hadi sasa katika mashindano yote wanayoshiriki kutokana na muunganiko wa kikosi chao.



Issa
Juve ubingwa wao