Ligi ya Uingereza inaendelea kusuka pesa za kutosha kwa sasa huku ikiendelea kuwalipa wachezaji wake vizuri ili kuwavuta waendelee kukaa katika vikosi vyao na kutoa huduma stahiki. Dili mbalimbali zikiwemo za kurekodi matangazo kwenye televisheni, kutanuka kwa namba ya mashabiki ambao wanaona kile kinachofanywa ni miongoni mwa vitu vinavyolipa sana. Pamoja na hilo wachezaji wengi wanapokea pesa nyingi ndani ya vilabu vyao kwa sasa wakiwemo:
Alexis Sanchez
Alipojiunga na United 2018 alipata uhamisho ambao kwa namna moja ulikuwa ni mwepesi sana kutokana na aina ya uchezaji wake kwa kipindi kile na uwezo aliokuwa nao mchezaji huyo. Ni Henrikh Mkhitaryan pekee alitosha kubadilishana na mchezaji huyo kutokana na biashara ambayo iliafikiwa baina ya wawili hao kutokana na ulazima wa Alexis kutaka kuhama. Kwa sasa anakula mshahara mkubwa sana ambao ni £391k kwa wiki pekee.
Mesut Ozil
Pamoja na sakata lake la chini linaloendelea kati yake na Unai lakini kwenye suala la malipo bado anakaa juu ndani ya klabu hiyo. Kwa sasa amekuwa sio chaguo la mwalimu na kupelekea hadi kutaka kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru kwa msimu uliopita. Naye analipwa kitita cha £350k kwa wiki pamoja na kukosa mechi nyingi za kucheza msimu huu.
Paul Pogba
Wengi walikuwa wakiona kwamba mchezaji huyo hakustahili kabisa kupokea kitita hicho cha hela kutokana na uchezaji wake alipokuwa chini ya utawala wa Mourinho lakini mambo yamekuwa tofauti kwa sasa hata vile watu wanaona anastahili sana kupokea kiwango hicho. Anapokea kiwango cha £290k kwa mwezi tu ndani ya klabu yake.
Kevin De Bruyne
Ni injini ya Man City kwa msimu huu na alifanya makubwa zaidi hata kwa msimu uliopita katika kampeni za kufukuzia ubingwa wa ligi. Amekuwa akifanya mambo makubwa katika safu ya kiungo jambo ambalo linamfanya Pep amuamini sana; analipwa mshahara wa £280k kwa mwezi akiwa anapewa pesa kubwa ndani ya klabu hiyo.
Mbali na hao kuna wachezaji wengine ambao wanakula mshahara mkubwa ndani ya klabu zao kutokana na uwezo na mchango wao lakini takwimu hizo zimetawaliwa sana na klabu mbili ambazo zina ushindani mkubwa kifedha. Wengine ni Raheem Sterling analipwa £275k kwa wiki, Romelu Lukaku £250k, Sergio Arguero anapokea £220k, Hary Kane analipwa £200k na Hazard ambaye Chelsea inamlipa £200k kwa wiki pekee.


Povel
Habar njema
Theckla
Hii imekaa safi Sana
Njiku
Ipo poa hii