Kwa mujibu wa meneja Pep Guardiola, Manchester city haiwezi kuwekwa kwenye levo za Real Madrid Barcelona au Bayern Munich ambao tayari wameshafikia sehemu fulani ya mafanikio.
Pep Guardiola ambaye kwa sasa ni mmoja wa mameneja ambao ni tishio kubwa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa anasema anaamini klabu yake ipo kwenye muelekeo mzuri kuelekea kuwa moja ya klabu boreaa duniani na pengine kuwafikia au kuwapita watangulizi wake.
Man City toka ilipokuwa mikononi mwa Sheikh Mansour mwaka 2008, wameweza kujiweka katika mazingira ya kuwa vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza sasa wakiwa wameshinda taji la ligi hiyo mara tatu.
Meneja Guardiola ambaye amewaongoza kwa misimu mitatu mpaka sasa ni mmoja kati ya mameneja bora zaidi wa kileo. Meneja huyu aliwasaidia Barcelona kushinda mataji matatu mwaka 2008-09 na kuwavutia klabu nyingi kubwa wakiwemo Bayern Munich ambako pia alishinda mataji matatu ya Bundasliga kabla hawajaenda Madrid.
Kwa uzoefu wa meneja huyu anaamini bado kuna mambo mengi ambayo Man City wanahitaji kuboresha na anaamini wapo kwenye njia sahihi ili waweze kuwa kwenye kundi moja au levo moja na klabu za Real Madrid Barcelona na Bayern Munich.
Guardiola anasisitiza kuwa hatua ndogo ndogo zitawapeleka mahalia ambapo wanapahitaji kufikika.

