Msemo unaotaja kuwa wanawake wakiwezeshwa wanaweza unaanza kupotea, msisitizo unawekwa katika usawa kwa jinsia zote mbili! Adidas hawako nyuma.
Jitihada za kusisitiza na kutetea usawa katika nyanja zote za maisha ndicho kinachotiliwa mkazo, Adidas nao hawapo nyuma kwa hili wametangaza kutoa malipo sawa ya bonasi kwa wanamichezo wa kike watakaoshinda Kombe la Dunia.
Kampuni hii kubwa ya vifaa vya michezo imetoa tangazo lake jana Ijumaa, siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambayo inaenda kwa kauli mbiu ya “malipo sawa kwa uchezaji sawa”.
Kampuni hii inaamini sasa umefika wakati ambao wanapaswas kutoa motisha kwa vizazi vinavyofuata wa wanamichezo wa kike na kuwatolea changamoto za kufanya vizuri zaidi.
Tangazo hili lianakuja wakati ambao wachezaji 28 wa timu ya wanawake ya Marekani wakiwa wamewasilisha madai dhidi ya shirikisho la soka la Marekani wakilalamikia kubagiliwa kijinsia.
Kukosekana kwa usawa kuna haribu utendaji katika na kufanya vizuri kuanzia kwenye mzaingira ya timu, malipo na kusafili kupata matibabu.


Povel
Habar njema
Frank Patrick
Imekaa vizuri sana hii kwa upande wa motisha
Issa
Imekaa poa