Mario Balotelli anataka kusalia Marseille

 

Mario Balotelli ameweka wazi kuwa anataka kuendelea kusalia Marseille hata baada ya msimu huu kuisha akisisitiza kuwa klabu hiyo ipo lrvo nyingine ukifnanaisha na Nice.

Balloteli alichapa jumla ya magoli 33 kwenye Ligue 1 kwa misimu yake miwili akiwa Nice lakini alishindwa kwenda sawa na bosi wa klabu hiyo akihusishwa na masuala ya afya wakati akishindwa kuona nyavu kwenye gemu 10 za Ligi mwanzoni mwa msimu.

Mwezi Januari ulimuacha Balotelli akiungana na klabu ya Marseille na kujikuta amerejea kwenye moto wake baada ya kuchapa magoli 4 kwenye gemu 4 za ligi kwa klabu hiyo mpya.

Wakijiandaa kuelekea kuchapana na klabu yake ya zamani Jumapili hii, Balotelli ameweka wazi kuwa angependa kuongeza mda wake wa kuendelea kuwepo klabuni hapo baada ya msimu huu kuisha.

“kiuhalisia mkataba wangu unafika tamati mwisho wa msimu huu, baada ya hapo tutajadili, nimemwambia wakala wangu ninafurahia kuwepo hapa nataka nibakie”

 

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Habari za kufurahisha

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.