Raha ya mechi ni ushindi siku zote lakini inapotokea upande mmoja unapoteza hugeuka na kuwa majonzi kwa wale wanaopoteza mechi husika. Hilo siku zote lipo na halizuiliki kabisa kutokana na kuwepo kwa aina tatu za matokeo uwanjani ambazo ni kushinda, kufungwa na kusuluhu. Hizi zote lazima ziwepo ili kuchochea ushindani katika soka.
Nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe bado haamini macho yake na kichwa chake kama kuna uhalisia juu ya mechi yao na United na kama walipoteza mechi hiyo. Suala hilo mara nyingi akilikumbuka linamnyima kabisa usingizi kutokana na uzito wa mechi hiyo na hatua waliyokuwa wameifikia wao kwenye mechi ya utangulizi.
Vijana hao wa Thomas Tuchel walitupwa nje ya michuano hiyo pamoja na kuingia katika mechi yao wakiwa kifua mbele kwa magoli 2-0 ambayo walipata ugenini lakini katika mechi ya marudio wakashindwa kuulinda ushindi huo na kujikuta wakiambulia kipigo cha 3-1 mbele ya vijana hao wa Ole Gunnar waliogeuka mwiba kwenye mechi ile ya marudio baada ya Rashford kuwapatia ushindi kupitia mkwaju wa penati.
Kitendo hicho ambacho PSG walikiangukia kwa mara ya pili katika historia yao ya hivi karibuni mbele ya Barcelona kimejirudia upya mbele ya United na kitu hiki lazima kiwakoseshe amani baadhi ya wachezaji kutokana na aina ya wachezaji walionao na uzito wa kikosi chao kwa mchezaji mmojammoja.
Mbappe anaendelea kulizungumzia hili kwamba imefikia wakati anakosa kabisa usingizi kutokana na mechi ile na ni imani yake kwamba kila mmoja kikosini pale lazima anajisikia vibaya baada ya kupata matokeo yale ya kushangaza ndani ya mechi yao. Haamini hilo kutokana na maandalizi waliyoyafanya kujijenga na mechi hiyo.
Pamoja na suala hilo wanasema ukiwa kama mchezaji lazima ukubali matokeo ili mambo mengine yaweze kuendelea; kwa kufanya hivyo itasaidia kumaliza msimu vizuri pamoja na maumivu hayo. Kwao kutolewa nje ya kichuano hiyo ni kovu lisiloponyeka maana lengo lao lilikuwa ni kufika mbali zaidi kwenye hilo.

Pamoja na kukosa nafasi kwa mwaka huu Mbappe ambaye Madrid wanamuwinda anaonelea kwamba bado wanayo nafasi kubwa kuendelea kufanya vizuri kwa misimu ijayo japo kwa msimu huu mambo yameenda sivyo na anachoamini kwa watakavyojipanga msinu ujao utakuwa mzuri sana Ufaransa.
Nyota huyo wa miaka 20 anaamini kikosi hicho kitaendelea kusalia hivyo na wachezaji wakaendelea kusalia kikosini hapo na nguvu ileile kama ilivyokuwa msimu huu. Pamoja na hayo yaliyowakuta anaamini kikosi hicho kitajirudi na kufanya maajabu ambayo wameyakosa kipindi cha mwanzo.


Neema juma
Asanteni kutujuza #meridianbet.
Fatina mfingi
Pole yake ndo mchezo