Kumbe Real Madrid ni Ndoto ya Pogba!

Kila mchezezaji mkubwa huwa na ndoto ambayo amekuwa akitamani kuitimiza kama mchezaji wa kulipwa, matamanio ya wachezaji hutofautiana na sio klia mchezaji huamua kuweka suala kama hilo wazi. Staa wa Manchester United Paul Pogba naye ni mmoja wa wachezaji ambao wanaiota ndoto ya siku moja kuchezea klabu ya Real Madrid.

Kiungo huyu ambaye ana umri wa miaka 26, amekuwa katika fomu nzuri zaidi klabuni United baada ya kufika kwa meneja wa mda bwana Ole Gunnar, nyota huyu anamsifia meneja huyu akidai wana uhusiano mzuri zaidi.

Akibainisha kuwa huenda na yeye siku moja akawa Real Madrid, Paul Pogba anasema kuwa Real Madrid ni klabu kubwa. Anasema japokuwa Real Madrid ni ndoto ya kila mchezaji kwa sasa yeye anafurahia kuwa United chini ya Ole Gunnar.

Kumbe Real Madrid ni Ndoto ya Pogba!

Wakati wa mwisho wa umeneja wa Jose Mourinho, Pogba alikuwa anahusishwa na kuihama klabu hiyo kwa sababu ya kutokuwa na uhusiano mzuri na meneja huyo aliyepita, huenda Real Madrid ambayo anaitaja kama ni klabu ya ndoto ya kila mchezaji ndiyo ambako angevutiwa kwenda.

Akimzungumzia Ole Gunnar

Pogba anaamini kuwa Ole Gunnar ni mwalimu bora kwa kipindi hiki akisisitiza kuwa yeye na wachezaji wengine wanafuraha kuwa chini yake.

Akiweka mkazo kuwa meneja huyu mwenye miaka 46, ameweza kurejesha matokeo mazuri klabuni hapo na kuwasaidia wachezaji kurudisha morali na kufurahia soka wanalolicheza. Anaamini Ole Gunnar anastahili kupewa kibarua cha kudumu, yeye na wenzake wangependa apewe kibarua cha kudumu.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Asantee kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe