Shirikisho la Soka Duniani, FIFA wamemfungia Kokou Hougnimon Fagla ambaye alikuwa ni refarii kujihusisha na soka kwa maisha yake yote baada ya kupatikana na hatia ya rushwa.
Kamati ya Maadili ya FIFA ilifungua uchunguzi mwezi machi mwaka jana baada ya Fagla ambaye alikuwa chini ya Shirikisho la Soka la nchini Togo kutuhumiwa kuwa alipokea rushwa kwaajili ya kupanga matokeo ya kirafiki ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa muamuzi huyu alishirikiana na Wilson Raj Perumal ambaye pia alikuwa anatuhumia kwa kupanga matokeo ya mechi za kimataifa kwa sababu shughuli za utabiri wa gemu hizo.

Tamko la Shilikisho la Soka Duniani linasema kuwa Fagla alikiuka utaratibu na sheria za FIFA hivyo uamuzi uliuofikiwa ni kumfungia muamuzi huyu kwa maisha yake yote asijihusishe na soka.


Neema hassan
Duuh..hatari
Povel tz
Duh majanga
Fatina mfingi
Haya majanga