Klabu Zilizofumania Sana Nyavu…

Mbali na klabu kuonesha kabumbu safi lakini pia jambo ambalo huonesha ubora halisi wa klabu husika ni suala zima la kufumania nyavu. Ili timu iwe bora zaidi inahitaji kufunga magoli mengi ambayo kwa hakika hushawishi uimara na ubora wa kila safu kuanzia safu ya ulinzi, ushambuliaji na muunganiko mzuri wa safu ya kiungo.

Kila klabu hupima uwezo wake kwa kuangalia idadi ya magoli waliyoweza kufunga na yale ambayo wao wameruhusu klabu pinzani ziweze kuwafunga. Kupitia hilo ni jambo la pekee sana kwa klabu kuwa na magoli mengi ya kufunga na wao kujilinda kwa kutokuruhusu magoli mengi ya kufungwa.

Leo tunakuwekea wazi takwimu ambazo zipo hadi sasa juu ya klabu ambazo zinaongoza kwa kuwa na magoli mengi kwenye msimu huu wa ligi jambo ambalo limewajengea heshima wao. Hii ni kwa klabu zote zinazopatikana kwenye ligi zote kubwa zinazofahamika duniani.

Ajax, wauaji hao wa klabu kubwa zenye majina kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu huu wamekuwa moto usiozimika na wanashika chati nyingine kwa kuwa na magoli mengi ndani ya msimu huu zaidi ya klabu nyingine yoyote ile inayoshiriki ligi. Hadi sasa wameweza kufunga magoli 155 katika mechi zao 51 ambazo wamecheza. Umakini na moyo wa kupambana ni vitu pekee ambavyo vimewasaidia kuweza kufika hatua hizo ambazo ndizo wanazivuka kwa nguvu kubwa sana.

Manchester City, wakiwa wanafukuzia taji la ligi kuu kwa sasa baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya bado wanakaa kwenye historia nzuri ya kuwa klabu inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli hadi sasa ndani ya ligi ya Uingereza lakini wakishika nafasi ya pili kwenye mjumuisho wa klabu zote duniani. Hadi sasa wana idadi ya magoli 154 ambayo wameyapata kwenye mechi zao 55 walizozicheza. Ambapo bado nyota wao Sergio Arguero anashika nafasi ya juu kabisa akiwa na magoli yake 30 katika michuano yote.

Paris Saint-Germain, sio jambo la kishangaza kuwakuta PSG katika nafasi hiyo kutokana na wachezaji alionao na uwezo wa kila nyota kwenye kikosi chao. Wamekuwa tishio kwenye kila mechi ambayo wanaingia uwanjani kuicheza. Ndani ya ligi wakiwa tayari na kapu la magoli 92 ambayo kwa uwiano huo ni kwamba miamba hao wa Ufaransa walikuwa wakifunga kila mechi waliyokuwa wanaicheza huku Mbappe akiongoza kundi la wafungaji kwa magoli yake 33.

Heko kwa Benfica na Ajax

Mbali na hao kuna klabu nyingine kama Barcelona wakiwa na magoli 125 kwenye mechi 51 walizocheza na Benfica magoli 118 kwenye mechi zao 51 ambazo wamezicheza uwanjani kwa msimu huu. Kwa hakika klabu kama Benfica na Ajax kwa msimu huu zimeonesha ukomavu wa aina yake kwa msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.