Hii inaweza kushangaza wengi kwamba kigezo kipi kimetumika kutambua nani anafanya vizuri katika msimu huu lakini siku zote ukweli haufichiki; pale mchezaji anapokuwa kwenye kiwango cha juu jambo hilo huonekana wazi kabisa machoni kwa kila mpenda soka na anayeshangilia ligi husika.
Majina yatakayotajwa sio mapya kabisa machoni mwa kila shabiki wa soka kutokana na kiwango bora kabisa kinachooneshwa na wachezaji hao. Wamekuwa msaada mkubwa sana kwa klabu zao na wengine hata upande wa timu zao za taifa wakisaidia timu hizo kufika hatua fulani ama kuondoka na alama kwenye mchezo wao. Baadhi yao ni:
Lionel Messi, kwa sasa anacheza akiwa hana upinzani kutoka kwa nyota mwenzake aliyeingia naye ushindani kwa kipindi kirefu sana. Lakini pamoja na hilo bado makali yake yanazidi kukua na kuongezeka kadri siku zinavyokwenda. Na mafanikio ya Barcelona hadi hapo walipo kwa sasa ni kwa sababu ya nyota huyo ambaye hadi sasa anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya msimu.
Cristiano Ronaldo, Juventus wanajivunia sana kuwa na mtu kama yeye kikosini kwao kutokana na mchango mkubwa ambao ameuweka hadi sasa kwenye kikosi hicho. Umri wake wa miaka 34 umekuwa sio kitu kwake kupata matokeo wakati wowote wanaotakiwa kupambana kama timu. Amejitahidi kuizoea ligi kwa kuzamisha magoli 19 ndani ya ligi jambo ambalo kwa mtu aliyeanza katika ligi mpya ni lenye mafanikio makubwa mno.
Raheem Sterling, ni miongoni mwa wachezaji wanaozungumziwa vibaya zaidi hata kwenye vyombo vya habari vya nyumbani: Sterling bado yupo kwenye nafasi nzuri sana msimu huu hasa kwenye kikosi chake cha Man City kutokana na mchango mkubwa anaoufanya kitu kinachoonesha kwamba anakua kisoka. Katika msimu huu amebadilika kwa kiwango kikubwa tofauti na misimu iliyopita akiwa na uwezo mzuri wa kupiga pasi na kufunga.
Neymar, pamoja na mambo ya kimaigizo anayoyafanya akiwa uwanjani lakini bado anapewa heshima yake ya kuwa mchezaji anayeisaidia klabu yake kupata matokeo uwanjani. Japo msimu huu hajaonekana sana viwanjani lakini katika mechi zake 23 alizocheza amezamisha magoli 20. Hili hajalionesha akiwa na PSG kwa kisingizio kwamba anacheza ligi ndogo: la hasha, pia, hata alipokuwa na Barcelona kule Hispania alikuwa mwiba kwa kiwango chake.
Uhamisho wake kutoka Southampton umeweza kuleta matunda makubwa sana kwa upande huu wa pili. Ameweza kuirudisha Liverpool kwenye kinyang’anyiro cha ushindani kwenye makombe yote makubwa wanayoshiriki kwa sasa. Pamoja na kukumbwa na majeraha ya baadhi ya wachezaji wa pembeni wa kikosi hicho lakini Van Dijk bado amebaki mhimili wa nafasi hizo zenye mapungufu kikosini hapo.


isha
Hongera nyingi sana kwao