Kila mchezaji huwa na nafasi kubwa ndani ya ligi yake na hata taifa kwa ujumla. Mengi anayoyafanya humkweza na kumfanya aonekane mwenye thamani na ushawishi mkubwa kisoka hata kwa wale wanaomfuatilia mchezaji huyo. Hilo hutokana na kupambana kwake, uwezo wa kufunga na kusaidia timu kwenye hali zote matokeo yanapohitajika.
Baadhi ya majina yanatajwa sana kwenye ligi kuu ya Uingereza kwamba yanaonekana kuwa na thamani kubwa na ushawishi mkubwa wa kithamani kutokana na uhitaji wa klabu nyingi duniani, mchango wao kwenye vikosi vya timu za taifa na mishahara wanayotafuna kwenye vilabu vyao. Baadhi ya nyota hao ni:
Nyota wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane anaonekana kuongoza kundi hili kwa kujinyakulia alama nyingi za kuonekana anafanya vizuri kwenye nafasi hiyo. Thamani yake inalinganishwa na £171M kitu ambacho ni kikubwa sana kwa nyota huyo wa Uingereza kutokana na ushindani mkubwa wa wachezaji ndani ya ligi hiyo.
Raheem Sterling naye anakaa kwenye kundi hilo akishikilia nafasi ya pili. Nyota huyo wa klabu ya Man City kwa sasa anaonekana kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho na thamani yake imekwishafika £161M.
Nyota hao wa Uingereza wanaonekana kuwa na thamani ya juu ndani ya ligi hiyo.
Afrika nayo hawapo mbali kwenye takwimu hizo. Mohamed Salah analinyanyua bara upande wa thamani zao ndani ya ligi wanazozichezea akikadiriwa kufikia £160M. Amekuwa mwiba sana kwenye ligi hiyo kutokana na mchango wake na uwezo wake unaoonekana kubadilika kila siku. Liverpool na Misri kwa nafasi zao wanajivunia sana kuwa na nyota wa aina yake.
Romelu Lukaku sio mchezaji wa maajabu sana ndani ya United lakini mchango wake ni mkubwa sana ndani ya kikosi cha taifa lake na wakati mwingine akiwa ndani ya United. Thamani yake na heshima yake bado ni msingi mkubwa ndani ya klabu hiyo. Anakadiriwa kufikia thamani ya £137M, kitu ambacho ni cha kipekee kwa maisha yake ya soka.
Eden Hazard anafuatia akiwa na thamani ya £105M kitu ambacho bado kinampa nguvu ya kuendelea kupambana ili kukaa nafasi za juu kabisa ndani ya ligi hiyo. Uwezo wake na thamani yake hakika havibezwi na mtu kwa sababu anafanya makubwa yanayoendana na kile anachopaswa kukifanya.
Nyota wengine ni kama vile Aubameyang – Arsenal (£72), Richarlison – Everton (£71M), Declan Rice – West ham (£71M), Tielemans – Leicester City (£52M), Mitrović – Fulham (£43M), Neves – Wolves (£40M), Ake – Bournemouth (£35M), Zaha – Crystal Palace (33M), Redmond -Southampton (£32M), Deulofeu – Watford (£32M).
Hao ni baadhi ya wengi wenye thamani za juu ndani ya ligi hiyo.


Christopher
bora angekuwa wa kwanza raheemm sterling , Kane ni forward wa msimu tu , injury nying
aisha
Pongezi kwake
Povel
Sterling yupo juuu hapo
Issa
Lazima wawe na thamani sana viwango vyao vipo juu