Lukaku Anatoa Sapoti kwa De Gea

Golikipa wa Man United ameendelea kuwa kuweka rekodi mbaya kwa kushindwa kulinda vyema lango na kuruhusu magoli ambayo yangeweza kuepukika. Lakini Romelu Lukaku anasema kuwa yupo pamoja na upande unatoa sapoti kwa mwanatimu mwenzake De Gea.

Man United walifanikiwa kupata goli la utangulizi, kwa kuwa mpira uliisha kwa bao 1-1, kama De Gea angeonesha umahiri wake vyema basi huenda sasa wangekuwa na matumaini zaidi ya kumaliza 4 bora.

Lukaku anasema yeye kwa mtazamo wake anaamini degea ni mchezaji anayefikilia zaidi mabadiliko chanya. Ni mtu anayeweza kujua makosa na kubadilika mapema sana.

“Magolikipa kuna mda mambo yanakuwa yanaenda vibaya sana. Kitu pekee unachoweza kufanya ni kufanya kazi kwa bidii. Sijui namna gani magolikipa hukipita kipindi hiki, mimi sio golikipa lakini, anafanya kazi kwa bidii kila siku.”

Golikipa wa Man United ameendelea kuwa kuweka rekodi mbaya kwa kushindwa kulinda vyema lango na kuruhusu magoli ambayo yangeweza kuepukika.
Lukaku kazini

United wanapoteza matumaini ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini Lukaku bado anaamini nafasi wanayo ya kufanya maajabu. “Hadi tushindwe kabisa, tunaamini hivyo daima klabuni hapa”

2 Komentara

    duuh pole yao

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe