Imekuwa ni vigumu kuamini kilichotokea katika mchezo wa nusu fainali iliyojenga historia ya aina yake kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya ambayo kwa hakika huwa na heshima ya pekee sana kisoka. Hata wenyeji wenyewe hawajaamini kama wamekamilisha hesabu hiyo ya kumuondoa Barcelona.
Uimara na umakini mkubwa wa Liverpool katika eneo lao la kiungo kwa hakika liliwaficha kwa kiwango kikubwa wageni hao na kuonekana kama sio wale waliozoeleka vizuri kugusa sana mpira wakiwa tayari na matokeo yanayomkingia kifua kufanya vizuri na kusonga mbele.
Kwa sasa Barcelona wamekuwa wahanga wakubwa sana wa kulinda matokeo kwenye michuano ya namna hii na hata kwenye mechi ya jana hawakuwa na nafasi ya kupewa heshima ya pekee ndani ya ligi ya hiyo ya mabingwa.
Inakumbukwa pia msimu wa 2018 Barcelona walitupwa nje na Roma kupitia aina hii ya ushindi ambayo iliwapa nafasi kubwa Barcelona kusonga mbele lakini walipokutana nchini Italia huku Roma akiwa nyuma kabisa alisawazisha makosa ya awali hadi kufikia hatua ya kumtoa nje ya michuano.
Pia, ndani ya msimu ameweza kukutana na tatizo linalorandana na hilo. Vilevile wameweza kututhibitishia usemi wa ‘kila mtu ashinde kwake’ kwamba Liverpool wameweza kukaa ndani ya nafasi yao ambayo huitwa namba 12 katika kuipa nguvu na matumaini ya kusonga mbele.
Historia maridadi
Alisson amekuwa mlinda mlango wa pekee ambaye ameshinda aina hii ya mechi kwa mara ya pili mbele ya Barcelona walewale. Ikiwa mara ya kwanza ilikuwa ni katika ushindi wa 4-1 akiwa na Roma na hii nyingine ni katika ushindi wa 4-0 akiwa na Liverpool. Ni mafanikio ya haraka sana.
Aina hii ya ushindi pia sio ya kwanza kwa Liverpool, kuweza kutoka nyuma ya matokeo mabovu na kufanya vizuri sana mbele ya mpinzani wake. Hili linatukumbusha miaka ya 2016 wakiwa na Dortmund walipindua meza kibabe sana; pia mwaka 2005 walifanya hivyo mbele ya miamba wa Italia, AC Milan.
Nani alaumiwe?
Barcelona hana wa kumlaumu zaidi ya uzembe wake mwenyewe ndani ya mechi hiyo kutokana na kujiachia sana na kuwa na falsafa ya ajabu ambayo ilishindwa kufanya kazi na hata kushindwa kubadilishwa. Coutinho amekuwa kama anapishana na gari la mshahara baada ya kuihama klabu yake hiyo lakini mwishowe ikafanya vizuri sana.
Wababe wa kufanya aina hiyo ya matokeo na wanaostahili pongezi za pekee ni wachezaji wote wa kikosi cha Liverpool lakini zaidi ni Origi na Wijnaldum aliyeingia kipindi cha pili na kubadili kabisa matokeo. Hawa wanatukumbusha ile fainali iliyochezwa Istanbul na akina Gerald kukiwa na aina hii ya matokeo ya kupindua meza bila ya baadhi ya baadhi ya nyota wao wa muhimu ndani ya kikosi chao.


isha
Duuh noma sana
Issa
Lazima wawike tu la massia