Ligi Kuu ya Uingereza inaheshimika kwa kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo wa kipekee sana na wanaotokea mataifa mbalimbali. Pia, inamiliki wachezaji ambao kwa upande mwingine wanaishia kusugua benchi katika ligi hiyo bila kuwa na historia nzuri ya wao kuweza kucheza soka lao siku za usoni. Baadhi ya nyota waliopoteza nafasi zao ndani ya ligi hizo ni:
Danny Welbeck, nyota huyo hadi inafikia wakati uwepo wake unasahaulika kabisa ndani ya klabu ya Arsenal. Hadi sasa amecheza michezo nane pekee akiwa na klabu yake hiyo ya Arsenal huku akiwa na umri wa miaka 28 ambao bado ni rafiki kwake kuendelea kufanya makubwa zaidi.
Emerson Hydman, klabu ya Bournemouth wanammiliki nyota huyo kwa kipindi chote tangu atue klabuni hapo hajawa na nafasi ya kuonesha uwezo wake wa kisoka zaidi ya kupotezwa kabisa na kuishia kusugua benchi. Akiwa na umri wa miaka 23 bado kabisa hajapata nafasi yoyote ya kuitumikia klabu hiyo msimu huu.
Danny Drinkwater, ni dhahiri kwamba nyota huyo atakuwa anayakumbuka maisha yake ya Leicester City baada ya kukosa kabisa nafasi ndani ya klabu hiyo. Ikumbukwe hawa ni miongoni mwa nyota ambao walinyanyua kombe wakiwa na klabu hiyo ya Leicester. Hadi sasa ndani ya msimu huu hajaingia kabisa uwanjani.
James McCarthy, ni wakati wa Roberto Martinez ambapo nyota huyo alikuwa akipata nafasi ya kucheza mechi zake ndani ya ligi hiyo lakini kwa sasa hajaweza kabisa kupata nafasi hiyo kwa kiwango kinachoridhisha. Ni nyota mwenye uwezo mkubwa lakini anashindwa kufanya makubwa kutokana na kunyimwa kabisa nafasi hiyo.
Danny Simpson, ndani ya klabu ya Leicester nyota huyo kwa hakika hajaweza kuonesha sana makali yake akiwa ameonekana uwanjani mara tano pekee katika umri wake wa miaka 32 aliyonayo pamoja na kuwa na uwezo wa kipekee sana ndani ya klabu yake hiyo. Kwa hakika anastahili zaidi kutokana na uwezo wake.
Alberto Moreno, inafika wakati hadi anasahaulika kabisa kutokana na kupotea machoni mwa mashabiki wengi wa soka. Ni mchezaji mwenye uwezo wa kipekee, anaweza kutengeneza nafasi akipewa namba ya kuonesha uwezo wake; jambo la kustaajabisha hadi sasa amecheza mechi mbili pekee kwa umri wake wa miaka 26 – sio kitu kizuri kabisa.
Fraser Forster, mlinda mlango mwenye heshima kubwa ndani ya ligi ya Uingereza na klabu ya Southampton kwa siku za nyuma, katika nyakati za hivi karibuni hajapata kabisa nafasi ya kuingia uwanjani kudhihirisha ubora wake akiwa kama mchezaji. Ni jambo la kushangaza kwa mchezaji wa aina yake kufanyiwa hivyo.
Vincent Janssen, kwa upande fulani tunaweza kusema hana bahati kutokana na namba anayoicheza klabuni hapo. Ni mbadala wa Harry Kane lakini ugumu ni kwamba kuna Llorente ambaye bado anaonekana kufanya vizuri kwenye nafasi hiyo hivyo kumfanya awe amecheza mechi moja pekee katika msimu huu!


Ernest
Danny Welbeck nyota yake ilizimika ghafla sana daah!!!
Povel
Gud news