Eden Hazard amekamilisha uhamisho wake kutoka Chelsea kwenda Real Madrid, akiongeza orodha ya wchezaji wakali walioandika historia kutoka Premier League kwenda La Liga.
Hazard anajiunga na mabingwa mara 13 wa Ulaya Real Madrid ambao wanatajwa kukubali kulipa ada ya paundi milioni 140. Anakuwa ni mchezaji wa mwisho kutoka EPL kwenda La Liga, dirisha bado liko wazi nani atamfuata?
Wachezaji kadhaa wa Ligi Kuu Uingereza wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye orodha ya kwenda kujiunga na La Liga. Tujikumbushe kwanza watangulizi wao;
Wachezaji matata ambao ni wa nyakati za hivi karibuni ambvao walitoka EPL kwenda La Liga ni pamoja na;
- Cristiano Ranoldo -Alisepa Manchester United Kujiunga na Real Madrid Julai 2009 kwa paundi milioni 94.
- Luka Modric alisepa Tottenham kwenda Real Madrid Agosti 2012 kwa paundi milioni 35.
- Gareth Bale alisepa Tottenham kwenda Real Madrid Septemba 2013 kwa paundi milioni 101.
- Luiz Suarez aliondoka Liverpool kwenda Barcelona Julai 2014 kwa paundi milioni 81
- Philippe Coutinho, alitoka Liverpool kwenda Barcelona, Januari 2018 kwa paundi milioni 130
Je nani atafuata?
Ripoti zinawataja mastaa kadhaa ambao wanahusishwa zaidi na klabu ya Real Madrid na Barcelon. Paul Pogba ni miungoni mnwa mastaa wanaozungumziwa zaidi, Christian Eriksen pia ameshaweka wazi kuwa atasepa Spurs na kuhusishwa sana na Real Madrid. Sadio Mane, David De Gea, Hary Kane na Alexandre Lacazette wote wapo kwenye orodha ambayo huenda wakamfuata Hazard hivi karibuni.


Njiku
Acha tuone