Mambo yanazidi kuwa matamu kuelekea Afcon 2019! Mashabiki 100 ambao wamesajiliwa wa timu ya taifa ya Ghana watapata fursa ya kusafiri kwenda Misri kushuhudia michuano ya Afcon 2019! Bajeti ya gharama za mashabiki hawa tayari imeshapitishwa na serikali ya Ghana.
Raisi wa umoja wa mashabiki/wadau wa timu ya taifa ya Ghana (Ghana Allience for Supporters Union) bwana Abraham Boakye amethibitisha suala hili akiwa anazungumza na kituo kimoja cha redio nchini humo.
Serikali ya nchi hiyo ipo tayari kudhamini gharama za mashabiki hawa za safari na uwepo wao nchini Misri kwa ajili ya michuano mapema mwezi huu, na tayari bajeti yao iko tayari.
Kwa sasa, timu ya taifa ya Ghana ipo jijini Abu Dhabi ndani ya Muungano wa Jumuiya ya Kiarabu ambako wanatarajiwa kutumia wiki tatu wakijinoa kuelekea michuano hiyo kabla hawajasafiri kutua Misri.
June 25, Ghana wataanza mechi yao ya ufunguzi dhdi ya Benin kwenye dimba la Ismaili Sports Stadium, kisha watakutana na Cameroon na Guinea Bissau kwenye Kundi F.
Chiku
Habari njema