Muarobaini wa United…

Manchester United wana maeneo mengi ambayo wanahitaji kuyafanyia marekebisho msimu huu na miongoni mwa eneo hilo ni lile la upande wa kulia ambalo limekuwa na matatizo sana katika kikosi hicho. Wao wapo mbioni kuangalia nani anayeweza kukaa kwenye nafasi hiyo na kuitumikia ili kuleta ushindani msimu ujao.

Ole Gunnar anatakiwa kufanya usajili ambao kwa hakika utakuwa na nguvu sana ili kurejesha ushindani kwenye ligi hiyo kutokana na kikosi hicho kuwa na matokeo ambayo hayakuwaridhisha wengi kwa siku za karibuni. Hadi sasa wakitaka kurejea sokoni vizuri kuna majina matano ambayo wanapaswa kuyaangalia ili kurejesha heshima:

Gareth Bale (Real Madrid), waliwahi kujaribu kumfukuzia nyota huyo hata kipindi cha nyuma wakihitaji huduma yake lakini hawakufanikiwa kutokana na masuala ya kimkataba ambayo nyota huyo alikuwa anakutana nayo na yalikuwa yanatakiwa kuendelea kumuweka kikosini hapo, anaweza kutoa msaada ndani ya United.

Jadon Sancho (Borussia Dortmund), ametoka kwenye timu ya watoto ya majirani zao Manchester City kabla ya kutimkia Dortmund. Ana uwezo wa aina yake ambao umewasaidia kwa kiwango cha pekee sana. Bila shida hata kung’ara kwa Pulisic ni mchango mkubwa sana wq mchezaji huyo. Kwa aina ya kiwango chake anaweza kuwa ni nguzo kubwa sana upande wa kulia wa timu hiyo.

Nicolas Pepe (Lille), amekuwa mwiba sana hadi kuanza kuwavuta wengi kuhitaji kumsajili. Kikosi chake kimekuwa na nguvu katika eneo hilo kutokana na uwezo wake aliouonesha. Uwepo wake kikosini umewasaidia Lille kucheza klabu bingwa.

Suso (AC Milan), nyota huyo wa miaka 25 amekuwa mwiba sana ndani ya kikosi hicho. Kiwango chake ni cha pekee sana na kwa kawaida ya soka la Italia na Uingereza lilivyo basi ni jambo kubwa sana kwake ili waweze kufanya vizuri. Kwa kiwango chake anaweza kuwa tunu kubwa sana ndani ya ligi hiyo.

David Neres (Ajax), ni jina ambalo limewaliza wakubwa sana ndani ya michuano ya klabu bingwa. Kuna kila linalowezekana kwamba United atakuwa na upinzani wa aina yake kumnasa. Kwa umri wake na kiwango chake ni tunu kubwa ya soka na inapaswa kuendelezwa.

2 Komentara

    Nikweli watafute mbadala alaka sana.

    Jibu

    United watulie kwenye uaajili sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.